1Ikawa katika mwezi wa Nisani wa mwaka wa ishirini wa mfalme Artasasta; hapo, mvinyo ilipowekwa mbele yake, nikaichukua hiyo mvinyo, nikampa mfalme; lakini mpaka hapo sijawa nikinuna mbele yake.
2Mfalme akaniuliza: Mbona uso wako unanuna, ukiwa huugui? Hili si jingine, ila ni sikitiko la moyo. Ndipo, nilipoingiwa na woga mwingi sana,
3nikamjibu mfalme: Mfalme na awe mwenye uzima kale na kale! Je? Uso wangu usinune, mji ulio na makaburi ya baba zangu ukiwa umebomoka, nayo malango yake yakiwa yameteketezwa kwa moto?
4Mfalme akaniuliza: Sasa wewe unatakaje? Ndipo, nilipomwomba Mungu wa mbinguni,
5nikamwambia mfalme: Vikiwa vema machoni pako, mfalme, mtumwa wako naye akiwa mwema machoni pako, nitume, niende katika nchi ya Yuda mle mjini mlimo na makaburi ya baba zangu, miujenge!
6Mfalme akaniuliza, naye mkewe alikuwa amekaa kando yake, kwamba: Safari yako itakuwa ya siku ngapi? Utarudi lini? Basi, mfalme akaviona kuwa vema, akanituma, nami nikaagana naye siku za kurudi.
7Kisha nikamwambia mfalme: Vikiwa vema kwake mfalme, na wanipe barua za kuwapelekea wenye amri walioko ng'ambo ya huko ya jito kubwa, waniache, nipite, mpaka nitakapofika Yuda.
8Tena barua kwa Asafu, mtunza miitu ya mfalme, anipe miti ya kutengeneza nguzo za malango ya boma lililoko penye hiyo Nyumba, nayo ya ukuta wa mji na ya nyumba yangu, nitakamoingia. Mfalme akanipa, kwa kuwa mkono wa Mungu wangu ulio mwema ulikuwa na mimi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.