Yosua 7 - Swahili Roehl Bible 1937

Wizi wa Akani unavumbuliwa.

1Wana wa Isiraeli wakakora manza kwa kuuvunja ule mwiko, kwani Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabudi, mwana wa Zera wa shina la Yuda, akachukua vitu vyenye mwiko; ndipo, makali ya Bwana yalipowawakia wana wa Isiraeli.

2Kisha Yosua akatuma watu kutoka Yeriko kwenda Ai ulioko karibu ya Beti-Aweni, upande wa maawioni kwa jua wa Beteli, akawaambia kwamba: Pandeni kuipeleleza nchi hiyo! Nao wale watu wakapanda kupeleleza Ai.

3Waliporudi kwa Yosua wakamwambia: Wasiende watu wote kupanda huko! Watu kama 2000 au 3000 watatosha, waupige Ai. Usiwasumbue watu wote pia! Kwani wao ni wachache.

4Kisha walipopanda kama watu 3000 kwenda huko, wakawakimbia watu wa Ai,

5nao watu wa Ai wakaua kwao kama 36, wakawakimbiza kuanzia kwenye lango la mji mpaka kufika Sebarimu, wakawaua huko penye mtelemko; ndipo, mioyo ya watu ilipoyeyuka kuwa kama maji.

6Naye Yosua akazirarua nguo zake, akajiangusha chini kifudifudi mbele ya Sanduku la Bwana mpaka jioni, yeye na wazee wa Waisiraeli, wakitia mavumbi vichwani pao.

7Kisha Yosua akaomba: Wewe Bwana Mungu, kwa nini umewavukisha watu hawa Yordani, ukitutia mikononi mwa Waamori, watuangamize? Ingetufaa sana kukaa ng'ambo ya huko ya Yordani!

8E Bwana! Nisemeje, kwa kuwa Waisiraeli wamewapa adui zao visogo?

9Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watakapovisikia, watatuzunguka, walitoweshe jina letu katika nchi hii. Nawe utafanya nini kwa ajili ya Jina lako kuu?

10Ndipo, Bwana alipomwambia Yosua; Inuka! Ni kwa sababu gani, ukianguka usoni pako?

11Waisiraeli wamekosa wasipolishika agano langu, nililowaagiza, kwa maana wamechukua vitu vyenye mwiko kwa kuviiba, wakavificha na kuvitia katika vyombo vyao.

12Kwa hiyo wana wa Isiraeli hawakuweza kusimama machoni pa adui zao, hawakuwa na budi kuwapa hao adui zao visogo, kwani wamejipatia kiapizo. Mimi sitaendelea kuwa nanyi, msipokitowesha hicho kiapizo katikati yenu.

13Inuka, uwaeue hawa watu na kuwaambia: Jieulieni siku ya kesho! Kwani hivyo ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Kiko kiapizo kilichoko katikati yenu, Waisiraeli; kwa hiyo hamtaweza kusimama machoni pa adui zenu, mpaka mkiondoe hicho kiapizo katikati yenu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help