5 Mose 12 - Swahili Roehl Bible 1937

Agizo la kuyakomesha matambiko yote ya kimizimu.

1Haya ndiyo maongozi na maamuzi, mtakayoyaangalia, myafanye katika hiyo nchi, Bwana Mungu wa baba zako atakayokupa, uichukue, iwe yako siku zote, mtakazoishi huku nchini.

2Sharti mpaangamize kabisa mahali pote, wamizimu mtakaowafukuza walipoitumikia miungu yao juu ya milima mirefu nako vilima, tena chini ya miti yenye majani mengi.

13Jiangalie, usitoe ng'ombe zako za tambiko za kuteketezwa nzima mahali po pote, utakapopaona!

14Ila mahali pale pamoja tu, Bwana atakapopachagua katika moja lao mashina yako, ndipo papasapo, utolee hapo ng'ombe zako za tambiko za kuteketezwa nzima, tena ndipo papasapo, uyafanye yote, mimi ninayokuagiza.

15Lakini roho yako ikiwa na uchu wa nyama tu, utazichinja na kuzila malangoni pako po pote kwa mbaraka ya Bwana Mungu wako aliyekupa hizo nyama; mwenye uchafu na mwenye kutakata atazila, kama ni za paa au kama ni za kulungu.

20Bwana Mungu wako atakapoipanua mipaka yako, kama alivyokuambia, nawe utakaposema: Nataka kula nyama, kwani roho yangu ina uchu wa nyama, basi, na ule nyama kwa huo uchu wote wa roho yako.

21Kama mahali pale, Bwana Mungu atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, patakuwa mbali kutoka kwako, basi, na utoe wa kuchinja katika ng'ombe wako au katika mbuzi na kondoo wako, Bwana aliokupa, ule nyama, kama nilivyokuagiza, malangoni pako, uukomeshe uchu wote wa roho yako.

22Kama nyama za paa na za kulungu zinavyoliwa, hivyo ndivyo, utakavyozila hizo nyama nazo, mwenye uchafu na mwenye kutakata watazila pamoja.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help