1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana kwamba:
2Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema kwamba: Yaandike hayo maneno yote, niliyokuambia katika kitabu!
3Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Tazama! Siku zitakuja, nitakapoyafungua mafungo yao walio ukoo wangu wa Isiraeli na wa Yuda, niwarudishe katika ile nchi, niliyowapa baba zao, nayo itakuwa yao tena; ndivyo, Bwana anavyosema.
4Haya ndiyo maneno, Bwana aliyoyasema kwa ajili ya Isiraeli na ya Yuda,
5kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Tumesikia sauti ya kustusha na kushangaza, hakuna penye utengemano.
6Ulizeni, mwone, kama yuko mwanamume atakayezaa! Mbona nimewaona waume wote wakitia mikono yao viunoni pao kama mwanamke anayetaka kuzaa? Mbona nyuso zote zimegeuka, zikachujuka?
23Mtakiona kimbunga cha Bwana, hata makaa yenye moto yakitoka kwake, nao upepo wa chamchela wenye nguvu utawaangukia vichwani wao wasiomcha Mungu.Yer. 23:19.
24Ukali wake Bwana wenye moto hautatulia, mpaka uyafanye na kuyatimiza mawazo ya moyo wake; siku za mwisho mtayatambua haya.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.