1Nakupenda kwa moyo, Bwana, uliye nguvu yangu.
2Bwana ni ngome yangu na boma langu, tena ni mponya wangu, ni Mungu aliye mwamba wangu, kwa hiyo ninamjetea; ni ngao yangu na pembe ya kunipatia wokovu, tena ni kingo langu.
20Yaupasayo wongofu wangu Bwana alinipa, akanipatia tena yaupasayo ung'avu wa mikono yangu.
21Kwani naliziangalia njia zake Bwana, nisifanye kilicho kiovu mbele yake Mungu wangu.
22Kwani maamuzi yake yote yako mbele yangu, nayo maongozi yake sikuyaacha, nisiyafuate.
31Kwani yuko nani aliye Mungu, asipokuwa Bwana? Tena yuko nani aliye mwamba, asipokuwa Mungu wetu?
32Ni yeye Mungu aliyenivika nguvu, njia yangu huitengeneza, iwe imenyoka kabisa.
33Hunipatia miguu ikimbiayo kama ya kulungu, anisimamishe kwangu vilimani juu.
34Huifundisha mikono yangu kupiga vita, mpaka mikono yangu iweze kupinda hata uta wa shaba.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.