1Nikasikia sauti kuu iliyotoka Jumbani mwa Mungu, ikiwaambia wale malaika saba: Nendeni, mvimwage nchini vile vyano saba vya makali ya Mungu!
3Wa pili alipokimwaga chano chake baharini, ndipo, ilipogeuka kuwa damu kama ya mfu; kwa hiyo vikafa mle baharini vyote vilivyokuwamo vyenye uzima.
4Wa tatu alipokimwaga chano chake katika mito na katika chemchemi za maji, ndipo, nayo yalipogeuka kuwa damu.Pigo la nne na la tano.
8Wa nne alipokimwaga chano chake juani, ndipo, lilipopewa kuwaunguza watu kwa moto.
9Lakini watu walipounguzwa kwa kuchomwa na moto sana wakalitukana Jina la Mungu aliyekuwa na nguvu ya mapigo hayo, wakakataa kujuta na kumtukuza yeye.
10Wa tano alipokimwaga chano chake kitini mwa kifalme mwa yule nyama, ndipo, ufalme wake ulipotiwa giza, wenyewe wakaziuma ndimi zao kwa kuumia sana,Pigo la sita na la saba.
12Wa sita alipokimwaga chano chake mle katika mto mkubwa wa Eufurati, ndipo, maji yake yalipokupwa, kusudi njia itengenezwe ya wafalme watakaotoka maawioni kwa jua.
17Wa saba alipokimwaga chano chake angani, ndipo, sauti kuu ilipotoka Jumbani mwa Mungu upande wa kiti cha kifalme ikisema: Imekwisha kufanyika!
18Kukapiga umeme na uvumi na ngurumo, kisha kukawa tetemeko kubwa la nchi kupita yote yaliyokuwapo; tangu hapo, mtu alipokaa nchini, halikuwapo tetemeko lililokuwa kubwa kama hilo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.