1 Timoteo 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuwaendea wazee na wajane wa kike kwa kuwaheshimu.

1Aliye mzee usimkaripie, ila umbembeleze, kama ni baba yako! Walio waume wazima useme nao, kama ni ndugu zako!Yawapasayo wazee.

17Wazee wanaosimamia vizuri sharti wapewe heshima mara mbili, kupita wengine ni wale wanaojisumbua kulitumikia lile Neno kwa kulifundisha.Tume. 14:23; Rom. 12:8.

18Kwani Maandiko yasema:

Ng'ombe mwenye kupura ngano usimfunge kinywa!

Na tena:

Mtenda kazi hupaswa na kupewa mshahara wake.5 Mose 25:4; Luk. 10:7; 1 Kor. 9:9.

19Mzee akisutwa, ukatae, wasipokuwapo mashahidi wawili au watatu!5 Mose 19:15; Mat. 18:16-17; 2 Kor. 13:1.

20Wakosao uwaonye mbele yao wote, wale wengine nao wapate kuogopa!Gal. 2:14.

21Namtaja Mungu na Kristo Yesu nao malaika waliochaguliwa kuwa mashahidi nikikuagiza sasa, uyashike maneno haya, nalo utakalolifanya lo lote, ulifanye pasipo kuchukizwa wala pasipo kupendezwa na mtu!

22Usimbandikie mtu mikono upesi! Wala usijitie katika makosa ya wengine! Jiangalie, uwe mng'avu!1 Tim. 4:14.

23Usifulize kunywa maji tu, ila utumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako, likipatwa na manyonge mara kwa mara!

24Watu wengine makosa yao yako waziwazi, huwaongoza na kuwapeleka penye hukumu; lakini wengine makosa yao hutokea nyuma yao.

25Vivyo hivyo nayo matendo mazuri mengine yako waziwazi; nayo yasiyo waziwazi hayafichiki.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help