1Yesu alipokwisha kuyasema haya akatoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito cha Kidoroni, kulikokuwa na kiunga. Humo wakaingia yeye na wanafunzi wake.(2-11: Mat. 26:47-56; Mar. 14:43-52; Luk. 22:47-53.)
2Lakini naye Yuda aliyemchongea alipajua hapo, kwani Yesu na wanafunzi wake walikusanyika mara nyingi hapo.Kukana kwa Petero.(12-27: Mat. 26:57-75; Mar. 14:53-72; Luk. 22:54-71.)
12Kisha kikosi cha askari na mkubwa wao na watumishi wa Wayuda wakamkamata Yesu, wakamfunga.
13Wakampeleka kwanza kwa Ana; kwani alikuwa mkwewe Kayafa aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule.
14Kayafa ndiye yule aliyekula njama na Wayuda kwamba: Inafaa, mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
33Pilato akaingia tena bomani, akamwita Yesu, akamwuliza: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda?
34Yesu akajibu: Wasema hivi kwa mawazo yako mwenyewe, au wako wengine waliokusimulia mambo yangu?
35Pilato akajibu: Je? Mimi Myuda? Wao wa taifa lako na watambikaji wakuu wamekuleta kwangu. Umefanya nini?
36Yesu akajibu: Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangeupigania, nisitiwe mikononi mwa Wayuda. Lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa.
37Pilato akamwuliza: Basi, wewe u mfalme gani? Yesu akajibu: Wewe unavyosema, ndivyo: mimi ni mfalme. Niliyozaliwa, tena niliyojia ulimwenguni, ndiyo hii: niishuhudie iliyo ya kweli! Kila aliye na kweli huisikia sauti yangu.1 Tim. 6:13.
38Pilato akamwambia: Iliyo ya kweli ndiyo nini? Alipokwisha kuyasema haya akawatokea tena Wayuda, akawaambia: Mimi sioni kwake neno la kumhukumu.
39Lakini iko desturi kwenu, niwafungulie mmoja siku ya Pasaka; basi, mwataka, niwafungulie mfalme wa Wayuda?
40Ndipo, walipopiga makelele tena wakisema: Huyu hatumtaki, twamtaka Baraba; naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.