1 Mose 21 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuzaliwa kwake Isaka.

1Bwana akamkagua Sara, kama alivyosema; naye Bwana akamfanyizia Sara, kama alivyomwagia.

14Kesho yake Aburahamu akaamka na mapema, akachukua mkate na kibuyu cha maji, akampagaza Hagari begani, kisha akampa na mwanawe; ndivyo, alivyompa ruhusa kwenda zake. Lakini alipokwenda akapotea katika nyika ya Beri-Seba.

15Maji yalipokwisha kibuyuni, akamwacha mwanawe chini ya kijiti,

16akaenda kukaa peke yake na kumwelekea mbali kidogo kama hapo, mtu anapotupa mshale kwa upindi, kwani alisema: Nisione, mwana anavyokufa! Alipokaa hivyo na kumwelekea akapaza sauti yake, akalia.

17Mungu alipokisikia kilio cha mtoto, malaika wa Mungu akamwita Hagari toka mbinguni, akamwambia: Una nini, Hagari? Usiogope! Kwani Mungu amekisikia kilio cha mtoto hapo, anapolala.

18Inuka, umwinue mtoto na kumshika kwa mkono wako! Kwani nitamfanya kuwa taifa kubwa.

19Kisha Mungu akamfumbua macho; ndipo, alipoona kisima cha maji, akaenda kukijaza kile kibuyu, akampa mtoto, anywe.

20Mungu akawa na huyu mtoto, akakua, akakaa nyikani, akawa mpiga upindi.

21Akakaa katika nyika ya Parani; naye mama yake akamwoza mwanamke wa nchi ya Misri.Maagano ya Aburahamu na Abimeleki.

22Ikawa wakati huo, ndipo, Abimeleki na Pikoli, mkuu wa vikosi vyake, walipomwambia Aburahamu kwamba: Mungu yuko pamoja na wewe katika mambo yote, unayoyafanya.1 Mose 26:26.

23Sasa niapie na kumtaja Mungu kwamba: Hutanidanganya mimi wala wao wa uzao wangu wajao nyuma yangu, ila huo wema, niliokufanyia wewe, unifanyie mimi nayo nchi hii, unayoikaa ugeni!1 Mose 20:15.

24Aburahamu akasema: Basi, mimi nitaapa.

25Kisha Aburahamu akamwonya Abimeleki kwa ajili ya kisima cha maji, watumishi wake Abimeleki walichokinyang'anya.1 Mose 26:15,18.

26Naye Abimeleki akasema: Simjui aliyelifanya jambo hilo, wewe nawe hujanipasha habari, mimi nami sijavisikia, ni leo hivi tu.

27Kisha Aburahamu akachukua mbuzi na kondoo na ng'ombe, akampa Abimeleki; hivyo ndivyo, wao wawili walivyofanya agano.

28Aburahamu akaweka wana kondoo saba peke yao,

29naye Abimeleki akamwuliza Aburahamu: Hawa wana kondoo saba ukiwaweka peke yao, ni wa nini?

30Akajibu: Hawa wana kondoo saba wa kike wachukue mkononi mwangu, upate kunishuhudia, ya kuwa nilikichimbua kisima hiki.

31Kwa sababu hii wakapaita mahali pale Beri-Seba (Kisima cha Kiapo), kwa kuwa waliapiana hapo wote wawili.1 Mose 26:33.

32Walipokwisha kulifanya agano hilo hapo Beri-Seba, Abimeleki na Pikoli, mkuu wa vikosi vyake, wakaondoka, wakarudi katika nchi ya Wafilisti.

33Aburahamu akapanda mvinje hapo Beri-Seba, akalitambikia hapo Jina la Bwana aliye Mungu wa kale na kale.1 Mose 12:8; Yes. 40:28; Rom. 16:26.

34Aburahamu akakaa ugenini katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help