2 Wakorinto 12 - Swahili Roehl Bible 1937

Kujivunia unyonge.

1Nashurutishwa kujivuna, hata isifae kitu. Lakini sasa nitafikia, nilivyotokewa na Bwana, nayo niliyofunuliwa.

2Yuko mtu nimjuaye kuwa mwenye Kristo; sasa miaka yapata 14, kama alikuwa mwilini, sijui, au kama alikuwa ametengwa na mwili wake, sijui; Mungu anayajua. Mtu huyo alipokonywa na kupelekwa, mpaka aiingie mbingu ya tatu.

3Nami nimemjua mtu huyo; kama alikuwa mwilini, au kama alikuwa pasipo mwili wake, sijui; Mungu anayajua.

4Naye alipokonywa kupelekwa Paradiso, akasikia maneno yasiyosemeka, yasiyowezekana kusemwa na mtu.

5Kwa ajili yake yeye nitajivuna, lakini kwa ajili yangu mimi hakuna, nitakalojivunia, isipokuwa unyonge wangu.Paulo anawafuata wao wenyewe, si mali zao.

11Nimekuwa mpuzi wa kujivuna, lakini ninyi mmenishurutisha. Kwani ingefaa, mimi nisifiwe nanyi. Kwani hakuna, nishindwacho nao wale wajipao macheo yote ya utume, hata nikiwa si kitu mimi.Makosa ya Wakorinto.

19Mmeanza kale kutuwazia, ya kuwa twajikania mbele yenu. Lakini Mungu ajua: twasema kwa kuwa wake Kristo. Nayo yote tunayasema, tuwajenge ninyi, wapenzi.

20Maana naogopa, ya kuwa nitakapokuja sitawaona ninyi, kama nitakavyo kuwaona, tena ya kuwa nami hamtaniona nanyi, kama mtakavyo kuniona. Naogopa kukuta magombano na wivu na mifundo ya mioyo na machokozi na masingizio na mateto na majivuno na matukutiko.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help