1Ikawa, mambo hayo yalipokwisha, wakamwambia Yosefu: Tazama! Baba yako ni mgonjwa. Ndipo, alipowachukua wanawe wawili Manase na Efuraimu kwenda naye.
2Walipompasha Yakobo habari kwamba: Tazama! Mwanao Yosefu anakuja kwako, Isiraeli akajitia nguvu, apate kukaa kitandani.
3Yakobo akamwambia Yosefu: Mwenyezi Mungu alinitokea Luzi katika nchi ya Kanaani, akanibariki,
8Isiraeli alipowaona wana wa Yosefu akauliza: Hawa ni nani?
9Yosefu akamwambia baba yake: Ndio wanangu, Mungu alionipa huku; ndipo, alipomwambia: Walete kwangu niwabariki!
21Kisha Isiraeli akamwambia Yosefu: Tazama! Mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, awarudishe katika nchi ya baba zenu.
22Nami nimekupa fungu moja zaidi ya ndugu zako, nililolichukua kwao Waamori kwa upanga wangu na kwa upindi wangu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.