1Mkono wa Bwana ukanishika, Bwana akanitoa kirohoroho, akanipeleka na kuniweka katikati ya hilo bonde, nalo lilikuwa limejaa mifupa.
2Akanipitisha po pote pande zote, ilipokuwa, nikaiona kuwa mingi sana humo bondeni juu ya mchanga, nami nikaiona kuwa mikavu sana.
3Akaniuliza: Mwana wa mtu, inakuwaje? Mifupa hii itaweza kuwa yenye uzima tena? Nikajibu: Bwana Mungu wewe unajua.
4Akaniambia: Ifumbulie mifupa hii yatakayokuwa! Iambie: Ninyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana!
5Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyoiambia mifupa hii: Tazameni, nitawaletea pumzi ndani yenu, mpate kuwa wenye uzima tena.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.