1 Mose 42 - Swahili Roehl Bible 1937

Safari ya kwanza ya kaka zake Yosefu.

1Yakobo alipoona, ya kuwa Misri vyakula viko, Yakobo akawaambia wanawe: Mbona mnatazamiana?

2Akasema: Tazameni, nimesikia, ya kuwa Misri vyakula viko! Telemkeni kwenda huko, mtununulie ngano huko, tupate kupona, tusife!

3Basi, kaka zake Yosefu kumi wakatelemka kununua ngano kule Misri.

4Lakini Benyamini, nduguye Yosefu, Yakobo hakumtuma kwenda na kaka zake, kwani alisema: Labda ataona kibaya njiani.

5Wana wa Isiraeli wakaingia katikati yao wengine waliokwenda kununua ngano, kwani njaa ilikuwa imeingia hata katika nchi ya Kanaani.

6Naye Yosefu alikuwa mtawala nchi hiyo, naye ndiye aliyewauzia ngano watu wote wa nchi hiyo. Kaka zake Yosefu walipofika kwake wakamwinamia, mpaka nyuso zao zikifika chini.

7Yosefu alipowaona kaka zake akawatambua, lakini akajitendekeza, kama hawajui, akasema nao maneno magumu, akawauliza: Mmetoka wapi? Wakasema: Tumetoka katika nchi ya Kanaani kuja huku kununua ngano.

8Ijapo Yosefu aliwatambua, wao hawakumtambua.

9Ndipo, Yosefu alipozikumbuka ndoto zake, alizoziota kwa ajili yao, kisha akawaambia: Mu wapelelezi, mmekuja kutazama, nchi hii inakokuwa wazi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help