Mashangilio 81 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumshukuru Mungu na kujuta.(Taz. Sh. 95.)

1Kwa mwimbishaji, wa kuimba kama wimbo wa wagemaji. Wa Asafu.

2Mpigieni Mungu shangwe, maana ni nguvu yetu! Mungu wa Yakobo mpigieni vigelegele!

3mwimbieni nyimbo za kumshukuru na kupiga patu! Pigeni nayo mazeze yaliayo vizuri pamoja na mapango!

4Pigeni mabaragumu, mwezi ukiandama! Hata penye mbalamwezi! Ndio sikukuu yetu.

9Sikilizeni, mlio wa ukoo wangu, niwaonye! Isiraeli, sharti unisikie!

10Kwako kusiwe tena na mungu mgeni! Wala usitambikie mungu wa nchi nyingine!

12Lakini walio ukoo wangu hawakuisikia hiyo sauti yangu, naye Isiraeli hakutaka kunifuata mimi.

13Nikawaacha, waufuate ugumu wao wa mioyo yao, wajiendee na kuyafanya mashauri yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help