1Miaka miwili ilipopita, Farao akaota, akajiona, akisimama kando ya mto.
2Akaona, ng'ombe saba wazuri mno walionona wakitoka mtoni, wakapanda kwenda kula majanini.
3Kisha akaona, ng'ombe saba wengine wakitoka mtoni kuwafuata wale, ni wabaya mno wenye nyama kavu, wakaenda kusimama kando yao wale ng'ombe wa kwanza ukingoni kwa mto.
4Kisha hawa ng'ombe wabaya wenye nyama kavu wakawala wale ng'ombe saba wazuri walionona; ndipo, Farao alipoamka.
5Alipolala tena usingizi akaota mara ya pili, akaona, masuke saba yaliyo manene na mazuri yakitoka katika bua moja.
6Kisha akaona, masuke saba mengine yakichipuka nyuma yao, nayo ni membamba kwa kunyaushwa na upepo wenye joto.
7Haya masuke membamba yakayameza yale masuke manene yaliyojaa ngano. Ndipo, Farao alipoamka, akaona, ya kuwa ameota.
8Kulipokucha akahangaika rohoni, akatuma kuwaita waaguaji wote walioko Misri na wajuzi wote wa ndoto; lakini Farao alipowasimulia ndoto zake, hakupatikana aliyemfumbulia Farao maana ya hizo ndoto.Yosefu anazifumbua ndoto za Farao.
9Ndipo, mkuu wa watunza vinywaji alipomwambia Farao kwamba: Leo hivi ninayakumbuka makosa yangu.
10Farao alipowakasirikia watumishi wake, alinitia katika kifungo nyumbani mwake mkuu wao wanaomlinda mfalme, mimi pamoja na mkuu wa wachoma mikate;
11ndipo, tulipoota ndoto usiku mmoja mimi na yeye, tulikuwa tumeota kila mtu ndoto yake yenye maana yake yeye.
12Basi, mle tulikuwa na kijana wa Kiebureo, mtumwa wake mkuu wao wanaomlinda mfalme; tulipomsimulia ndoto zetu, akamfumbulia maana yao, kila mtu akamfumbuli ndoto yake yeye.
13Navyo, alivyotufumbulia, vikawa hivyo; mimi walinirudisha katika kazi, naye mwenzangu akanyongwa.
14Ndipo, Farao alipotuma kumwita Yosefu; wakamfungua upesi mle kifungoni, akajinyoa nywele, akavaa nguo nyingine, kisha akaja kuingia kwake mfalme.
15Farao akamwambia Yosefu: Nimeota ndoto, lakini hakuna anayezifumbua. Nimesikia habari yako kwamba: Unaposikia ndoto huifumbua.
16Yosefu akamjibu Farao kwamba: Sio mimi, Mungu na ayafunue yatakayompatia Farao utengemano!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.