1Bwana akamwambia Mose kwamba:
2Waambie wana wa Isiraeli, wanichangie vipaji vya tambiko, mtoze kila mtu, kama moyo wake unavyomtuma.Sanduku la Agano.(10-22: 2 Mose 37:1-9.)
10Tengenezeni sanduku la mbao za migunga, urefu wake uwe mikono miwili na nusu, nao upana wake uwe mkono mmoja na nusu, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mkono mmoja na nusu.
11Ulifunikize lote dhahabu tupu, upande wa ndani na wa nje uufunikize hivyo, kisha uzungushe juu yake taji la dhahabu.
12Tena utengeneze mapete manne kwa kuyeyusha dhahabu, uyatie penye pembe zake nne, mapete mawili upande wake mmoja, tena mapete mawili upande wake wa pili.
13Kisha utengeneze mipiko miwili ya migunga, nayo ifunikize dhahabu,
14kisha hiyo mipiko itie katika yale mapete pande zote mbili za sanduku, iwe ya kulichukulia hilo sanduku.
15Namo katika hayo mapete ya sanduku mipiko sharti ikae humo, isitoke humo.
16Namo sandukuni uuweke Ushahidi, nitakaokupa.Kiti cha Upozi.
17Kisha utengeneze kifuniko cha dhahabu tupu kuwa Kiti cha Upozi, urefu wake uwe mikono miwili na nusu, nao upana wake uwe mkono mmoja na nusu.Kinara kikubwa.(31-39: 2 Mose 37:17-24.)
31Tena utengeneze kinara cha dhahabu tupu! Hiki kinara na kitengenezwe kwa kufuafua dhahabu, ipate kutoka shina lake na mti wake, navyo vikombe vyake na vifundo vyake na maua yake, vyote pia viwe vimetoka katika dhahabu iyo hiyo moja.
32Matawi sita na yatoke penye mbavu zake, matawi matatu ya kinara na yatoke penye ubavu mmoja, tena matawi matatu ya kinara na yatoke penye ubavu wa pili.
33Vikombe vitatu vinavyofanana na maua ya mlozi viwe katika kila tawi moja, yaani vifundo pamoja na maua yao. Vivyo hivyo katika matawi yote sita yanayotoka katika mti wa kinara.
34Lakini katika mti wa kinara viwe vikombe vinne vinavyofanana na maua ya mlozi, yaani vifundo pamoja na maua yao.
35Tena kila mahali, matawi mawili yanapotoka katika huo mti wake, chini yake kiwe kifundo kimoja. Viwe vivyo hivyo kila mahali, matawi mawili yanapotoka. Nayo matawi yanayotoka katika kinara yawe sita.
36Vifundo na matawi yao sharti yote yawe kazi moja iliyoyatokeza yote pamoja kwa kuifuafua dhahabu iyo hiyo moja, nayo yawe dhahabu tupu.
37Kisha utengeneze taa zake saba, nazo hizo taa zake uziweke juu yake, zipaangaze mahala palipo mbele yake.
38Nazo koleo zake na makato yake yawe ya dhahabu tupu.
39Sharti ukitengeneze pamoja na hivi vyombo vyake vyote kwa kipande cha dhahabu chenye uzito wa mizigo miwili.
40Angalia, uyafanye yote kwa mfano, niliokuonyesha mlimani!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.