Yesaya 12 - Swahili Roehl Bible 1937

Wimbo wa shukrani wa Wasioni waliookoka.Siku ile utasema:

1*Nakushukuru, Bwana, ya kuwa ulinichafukia,

kwani machafuko yako yamegeuka, ukanituliza moyo.

2Mtazamieni Mungu aniokoaye!

Pasipo woga wo wote ninamngojea,

kwani Bwana ni nguvu yangu na shangilio langu,

yeye Bwana ndiye aniokoaye.

3Kwa furaha mtachota maji visimani kwenye wokovu.

4Siku ile mtasema:

Mshukuruni Bwana, nalo Jina lake litambikieni!

Yajulisheni makabila ya watu matendo yake!

Wakumbusheni kwamba: Jina lake ni boma!

5Mshangilieni Bwana! Kwani hufanya makuu.

Hayo sharti yajulikane katika nchi zote!

6Pigeni shangwe na vigelegele, ninyi mkaao Sioni!

Kwani aliye mkuu kwenu katikati ndiye Mtakatifu wa Isiraeli.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help