Mashangilio 63 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuwa na Mungu kunapita mengine yote.Wimbo wa Dawidi, alioutunga alipokuwa nyikani kwa Yuda.

1Mungu, wewe u Mungu wangu, ninakutafuta mapema; roho yangu ina kiu ya kunywea kwako, nazo nyama za mwili wangu zinakutunukia sana, hapa katika nchi kavu ichokeshayo kwa kuwa pasipo maji.1 Sam. 22:5; 23:14; 24:1; Sh. 42:3; 143:6.

2Hivyo ndivyo, nilivyokutazamia Patakatifu pako, niione nguvu yako na utukufu wako.

3Kwani upole wako ni mwema kuliko uzima; kwa hiyo midomo yangu sharti ikusifu.

4Hivyo nitakutukuza siku zangu zote, nitakazokuwapo, Jina lako nitaliinulia mikono yangu.

5Hivi vinaishibisha roho yangu kama kiini cha mafuta, midomo yangu ikikupigia vigelegele, kinywa changu kikikushangilia.

6Ninapokwenda kulala ninakukumbuka, napo ninapoamka ninayawaza mambo yako.

7Kwani wewe ndiwe uliyenisaidia, namo kivulini mwa mabawa yako ninapiga shangwe.

8Roho yangu inagandamana nawe wewe, mkono wako wa kuume ukanishikiza.

9Lakini wao wanaoitafuta roho yangu, waiangamize, sharti washuke kuzimuni huko ndani ya nchi.

10Watu watawatoa, wauawe kwa ukali wa panga, kisha watakuwa chakula chao mbwa wa mwitu.

11Lakini mfalme atafurahia kuwa wake Mungu, wote wamwapiao yeye watashangilia, kwani vinywa vyao wasemao uwongo vitafumbwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help