Mashangilio 8 - Swahili Roehl Bible 1937

Udogo na ukuu wa mtu.Kwa mwimbishaji, wa kuimba kama wimbo wa wagemaji. Wimbo wa Dawidi.

1Bwana Mungu wetu, Jina lako hutukuka sana katika nchi zote, maana umeutanda utukufu wako kule mbinguni.

2Vinywani mwao watoto wachanga namo mwao wanyonyao ulijitengenezea tukuzo, upate kuwashinda wao wakupingiao, upate kumnyamazisha hata mchukivu naye ajilipizaye.

5Ulimpunguza kidogo, asilingane na wewe, Mungu, lakini macheo na mapambo yenye utukufu ndiyo, uliyomvika.1 Mose 1:26.

6Ukampa kuyatawala yote, mikono yako iliyoyafanya, yote pia ukayaweka kuwa chini miguuni pake:Mat. 28:18; 1 Kor. 15:27.

7kondoo na ng'ombe wote pamoja, nao nyama wa porini,

8hata ndege wa anga nao samaki wa baharini, nao nyama wote waliomo vilindini mwa bahari.

9Bwana Mungu wetu, Jina lako hutukuka sana katika nchi zote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help