Ezekieli 45 - Swahili Roehl Bible 1937

Mafungu ya nchi yapasayo Patakatifu na watambikaji na Walawi na wakuu.

1Mtakapopiga kura za kujigawanyia mafungu ya nchi hii, mtatoa kwanza katika nchi hii kipande cha kumpa Bwana kuwa Patakatifu, urefu wake uwe mianzi 25000, nao upana wake uwe mianzi 10000; hapo sharti pawe Patakatifu katika mipaka yake yote ipazungukayo!

2Ndani yake pakatwe mahali penye mianzi 500 pande zake nne zipazungukazo kuwa pake Patakatifu Penyewe; mahali hapo pazungukwe pande zote na uwanda wa mikono 50.

3Mahali hapo palipopimwa utapapima tena urefu wa mianzi 25000 na upana wa mianzi 10000, napo hapo ndipo pajengwe Patakatifu patakapokuwa Patakatifu Penyewe.

4Nchi hiyo itakuwa takatifu, iwe yao watambikaji wanaofanya kazi za utumishi wa Patakatifu wakimkaribia Bwana na kumtumikia; kwa hiyo mahali hapo patakuwa pao pa nyumba zao, napo patakuwa patakatifu penye hapo Patakatifu.

5Pengine penye urefu wa mianzi 25000 na upana wa mianzi 10000 patakuwa pao Walawi wanaofanya kazi za utumishi wa Nyumba hii; hapo patakuwa mali zao za kupashika kuwa pao pa kukaa penye matuo 20.

6Kisha mtatoa tena mahali penye upana wa mianzi 5000 na urefu wa mianzi 25000 kuwa pake mji, pawe kandokando ya kile kipande kitakatifu cha nchi; hapo patakuwa mali zao wote walio mlango wa Isiraeli.

7Naye mkuu mtampa huku na huko penye kile kipande kitakatifu napo penye pake mji mbele ya kipande kitakatifu na mbele ya hapo palipo pake mji paelekeapo baharini upande wa kwenda baharini napo paelekeapo maawioni kwa jua, urefu wake ulingane na urefu wa fungu moja wa mafungu ya mashina toka mpaka wa baharini hata mpaka wa nchi uelekeao maawioni kwa jua.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help