Waroma 1 - Swahili Roehl Bible 1937

Anwani.

1Mimi Paulo nilye mtumwa wa Kristo Yesu nimeitwa kuwa mtume kwa hivyo, nilivyochaguliwa, niutangaze Utume mwema wa Mungu.Nguvu ya Utume.

8Kwanza ninamshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu ninyi nyote, kwa kuwa hivyo, mnavyomtegemea, hutangazwa ulimwenguni mote.

13*Lakini ndugu zangu, sitaki, mkose kujua, ya kuwa nilijielekeza mara nyingi, nije kwenu, nione pato hata kwenu, kama nilivyoliona kwa wamizimu wengine; lakini nimezuiliwa mpaka leo hivi.

14Nimeingia udeni kwa Wagriki hata kwa washenzi, kwa wajuzi hata kwa wapuzi.

15Kwa hivyo, nilivyo mimi, nimekwisha kujifunga, niwapigie nanyi ile mbiu njema huko Roma.

16Maana sioni soni ya kuutangaza Utume mwema wa Kristo, kwani unayo nguvu ya Mungu ya kuwaokoa wo wote wanaoutegemea, kwanza Wayuda, kisha Wagriki nao.Makosa ya wamizimu.

18Kwani makali ya Mungu yanashuka toka mbinguni, yawatokee watu wote wasiomcha Mungu nao wenye upotovu, wanaoyazuia yaliyo ya kweli kwa upotovu wao;

19kwani mambo ya Mungu yametambulikana kwao, maana yalifumbuliwa, naye Mungu ndiye aliyewafumbulia.

24Kwa hiyo Mungu akawatupa, wajichafue wakizifuata tamaa za mioyo yao na kujipujua, mpaka wakifujiana miili yao wao kwa wao;Tume. 14:16.

25ni wao hao walioigeuza kweli ya Mungu kuwa uwongo, wakakitambikia kiumbe na kukitumikia kuliko Muumbaji aliye mwenye kutukuzwa kale na kale. Amin.

26Kwa hiyo Mungu aliwatupa, waingiwe na tamaa za upujufu. Kwani hata wanawake wao wakayageuza matumikio yao ya kimtu, wakazusha mengine yasiyo ya kimtu.

27Vile vile hata waume wakaacha kuwatumia wanawake kimtu, tena kwa hivyo, tamaa zao zilivyowachoma kama moto, wakatumiana waume na waume wenzao; wakafanya hayo yasiyopasa kamwe, wakapata malipo ya upotevu wao yaliyowapasa.3 Mose 18:22; 20:13; 1 Kor. 6:9.

28Tena kwa hivyo, walivyokataa kumshika Mungu na kumtambua, Mungu aliwatupa, wafuate mawazo ya ujinga na kufanya yasiyompasa mtu.

29Wakaenea upotovu wote na ubaya na choyo na uovu, wakajaa kijicho na uuaji na magombano na manyatio na mazoezo maovu.

30Ndio watetaji, wabishi, wasingiziaji, wenye kumbeza Mungu na kubeza watu, wenye kujivuna na kujitukuza, wenye maoneo maovu na wenye kuwakataa wazee.

31Hawana utambuzi wala welekevu wala upendo wala huruma.

32Nao walikuwa wameyambua yaliyoongoka mbele ya Mungu kwamba: Wanaoyatenda mambo hayo wamepaswa na kuuawa; tena hawayafanyi tu hayo, lakini nao wengine wakiyatenda, wanapendezwa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help