1Kisha Mose akatoka kwenye mbuga za Moabu, akaupanda mlima wa Nebo ulio mrefu zaidi kuliko milima mingine ya Pisiga, unaoelekea Yeriko. Huko Bwana akamwonyesha nchi yote ya Gileadi mpaka nchi ya Dani,
7Mose alikuwa mwenye miaka 120 alipokufa, macho yake yalikuwa hayakufifia, nazo nguvu zake za mwilini zilikuwa hazikupunguka.
8Wana wa Isiraeli wakamwombolezea Mose siku 30 katika mbuga za Moabu, hata siku za maombolezo ya matanga ya Mose zikatimia.
10Kwao Waisiraeli hakuinuka tena mfumbuaji kama Mose, Bwana aliyejuana naye uso kwa uso,2 Mose 33:11; 4 Mose 12:6-8.
11wala hakuna aliyefanana naye kwa kufanya vielekezo na vioja vyote, Bwana alivyomtuma katika nchi ya Misri kumfanyizia Farao nao watumishi wake wote na wenyeji wote wa nchi yake,
12wala hakuna aliyefanana naye kwa kufanya matendo yote ya nguvu za mikono yake wala kwa yale makuu yote ya kustusha, Mose aliyoyafanya machoni pao Waisiraeli wote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.