1Okoa, Bwana! Kwani wamekwisha wao wakuchao, nao wakutegemeao wametoweka kwenye wana wa watu.
2Kila mtu na mwenzake husemeana yaliyo uwongo, midomo yao husema yenye ujanja, kwa kuwa wenye mioyo miwili.
3Bwana na akomeshe midomo yote yaliyo yenye ujanja, nazo ndimi zisemazo maneno makuu tu!
4Ndio wanaosema: kwa nguvu za ndimi zetu tutashinda sisi, nayo mikono yetu hutusaidia; yuko nani atakayetutawala?
5Kwa ajili ya taabu zao walio wanyonge na kwa ajili ya yowe zao walio wakiwa nitainuka sasa, ndivyo, Bwana asemavyo, niwapatie wokovu wauchuchumiao.
6Maneno ya Bwana ndiyo maneno yaliyo mang'avu hufanana na fedha zilizoyeyushwa chunguni huku nchini, zilizong'azwa hivyo mara saba.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.