1Nimekuwa nimemngojea yeye Bwana, naye akaniinamia, akakisikiliza kilio changu.
2Akanitoa katika mwina uangamizao, nako kwenye matope yazamishayo, akaisimamisha miguu yangu juu mwambani, nao mwendo wangu akaushupaza.
3Akanipa kinywani mwangu wimbo mpya, nao ni wa kumshangilia Mungu wetu. Wengi wataviona na kuogopa, kisha nao watamwegemea huyu Bwana.
4Mwenye shangwe ni mtu amtumiaye Bwana kuwa egemeo lake, asiyewageukia wajivunao, wala wao wanaodanganya na kutumikia uwongo!
5Bwana Mungu wangu, uliyoyafanya wewe, ni mengi, ni mataajabu yako na mawazo yako yaliyotutokea; hakuna anayefanana nawe wewe. Ninataka kuyatangaza na kuyasimulia, ijapo yawe mengi, yasihesabike.
6Ng'ombe na vyakula vya tambiko hakupendezwa navyo, lakini umenizibua masikio yangu; ng'ombe za tambiko zinazoteketezwa nzima navyo vipaji vya tambiko vya kulipa makosa hukuvitaka.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.