Mpiga mbiu 4 - Swahili Roehl Bible 1937

Huku nchini hakuna kutulia.

1Nilipoyatazama tena makorofi yanayofanywa chini ya jua, niliona machozi yao waliokorofishwa, lakini sikuona aliyewatuliza mioyo; namo mikononi mwao waliowakorofisha zimo nguvu, kwa hiyo kwao hakuna atakayewatuliza mioyo.

2Kwa sababu hii nikawawazia wafu waliokufa kale kuwa wenye shangwe kuliko wao wanaoishi bado wenye maisha.

4Tena niliona, ya kuwa masumbuko yote na kufanikiwa kote katika kazi hutoka katika wivu, mtu anaomwonea mwenziwe; hayo nayo ni ya bure na kuukimbilia upepo.

5Mjinga hukaa na kuifunga mikono yake; basi, hujila mwenyewe.

7Nikatazama na mengine yaliyo ya bure chini ya jua:

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help