1Samusoni alipokwenda Gaza akaona huko mwanamke mgoni, akaingia kwake.
2Wagaza walipoambiwa, ya kuwa Samusoni ameingia humo, wakaizunguka hiyo nyumba na kumvizia usiku wote penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha kwa kwamba: Tungoje mapambazuko ya asubuhi, tupate kumwua.
3Lakini Samusoni akalala mpaka usiku wa manane tu; hapo usiku wa manane ndipo, alipoondoka, akaishika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo, akajitwika mabegani, akaipandisha mlimani kunakoelekea Heburoni.
4Ikawa baadaye, Samusoni akapenda mwanamke aliyekaa penye kijito cha Soreki, jina lake Delila.
5Ndipo, wakuu wa Wafilisti walipopanda kufika kwake, wakamwambia: Umnyenge, upate kuona, nguvu zake kubwa zilimo, tena utazame njia ya kumwona sisi, tupate kumfunga na kumshinda. Kisha tutakupa kila moja fedha elfu moja na mia moja.
18Delila alipoona, ya kuwa amemjulisha yote yaliyokuwamo moyoni mwake, akatuma kuwaita watu wa Wafilisti kwamba: Pandeni mara hii tu! Kwani amenijulisha yote yaliyokuwamo moyoni mwake. Nao wakuu wa Wafilisti walipopanda kufika kwake walishika zile fedha mikononi mwao.
19Kisha akambembeleza, alale usingizi penye magoti yake; alipokwisha akaita mtu, naye akazinyoa zile chungu saba za kichwani pake; ndivyo, alivyoanza kumshinda, maana nguvu zake zilikuwa zimemtoka.
20Kisha akasema: Wafilisti wanakujia, Samusoni. Alipoamka katika usingizi, alisema moyoni: Nitatoka kama mara nyingine zote kwa kujinyosha tu, kwani hakujua, ya kuwa Bwana ameondoka kwake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.