1Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wana wa Isiraeli wakakusanyika wakifunga mfungo na kuvaa magunia na kujitia mchanga vichwani.
2Waliokuwa wa uzao wa Kiisiraeli wenyewe wakajitenga na wenzao wote wa kabila jingine, kisha wakasimama wakiyaungama makosa yao na maovu, baba zao waliyoyafanya.
3Wakainuka, wasimame hapohapo, walipokuwa, wakasoma katika kitabu cha Maonyo ya Bwana Mungu wao saa tatu, saa tatu nyingine wakaungama na kumwangukia Bwana Mungu wao.
4Kisha Yesua na Banai, Kadimieli, Sebania, Buni, Serebia, Bani na Kenani wakatokea wakisimama hapo juu, Walawi wanaposimama, wakamlilia Bwana Mungu wao kwa kupaza sauti sana.
5Kisha Walawi Yesua nao Kadimieli, Bani, Hasabunia, Serebia, Hodia, Sebania na Petaya wakawaambia: Inukeni, mtukuzeni Bwana aliye Mungu wenu tangu kale hata kale! Watu na walitukuze Jina lako tukufu lililo kuu kupita matukuzo yote na sifa zote.
6Bwana, wewe ndiwe peke yako; wewe uliziumba mbingu, hizo mbingu zilizoko juu kuliko mbingu zote na vikosi vyao vyote, hata nchi nayo yote yaliyoko, hata bahari nayo yote yaliyomo; wewe ndiwe unayewapa wao wote kuwa wenye uzima, navyo vikosi vya mbinguni hukuangukia.
7Bwana Mungu, wewe ndiwe uliyemchagua Aburamu, ukamtoa Uri kwao Wakasidi, ukampa jina la Aburahamu.
9Ulipoyaona mateso ya baba zetu katika nchi ya Misri, ukavisikia vilio vyao kwenye bahari ya Ushami,
16Lakini wao baba zetu wakajikuza, wakazishupaza kosi zao, hawakuyasikia maagizo yako.
26Lakini wakakataa kutii, wakakuinukia, wakayatupa Maonyo yako nyuma yao, nao wafumbuaji wako wakawaua, kwa kuwa waliwaumbua kwa ushuhuda wao, wawarudishe kwako, wakasema masimango makuu.
27Kwa hiyo ukawatoa na kuwatia mikononi mwao waliowasonga, wakawasonga kweli; lakini hizo siku za kusongeka kwao walipokulilia, ukawasikia toka mbinguni, tena kwa huruma zako nyingi ukawapatia waokozi, wakawaokoa mikononi mwao waliowasonga.
32Sasa Mungu wetu uliye Mungu mkuu mwenye uwezo wa kutia woga, unashika maagano ya upole! Yasiwe madogo mbele yako masumbuko yote yaliyotupata sisi, wafalme wetu na wakuu wetu na watambikaji wetu na wafumbuaji wetu na baba zetu nao wote walio ukoo wako tangu hapo, wafalme wa Asuri walipotujia hata siku hii ya leo.Neh. 1:5.
33Wewe u mwongofu katika hayo yote yaliyotujia, kwani ulifanya yaliyo kweli, lakini sisi tukafanya maovu.Ezr. 9:15; Dan. 9:5,7.
34Nao wafalme wetu na wakuu wetu na watambikaji wetu na baba zetu hawakuyafanya Maonyo yako, masikio yao hawakuyategea maagizo yako wala ushuhuda wako, uliowashuhudia.
35Ijapo uliwapa ufalme wao, ukawatolea wema wako mwingi, ukawapa nchi kubwa yenye vinono, waione na macho yao, lakini wao hawakukutumikia, wala hawakurudi na kuyaacha matendo yao mabaya.
36Kwa hiyo sisi tu watumwa katika nchi, uliyowapa baba zetu, wayale mazao yake na mema yake, tazama, kuku huku sisi tu watumwa.
37Mapato yake mengi ni yao wafalme, uliotupa, watutawale kwa ajili ya makosa yetu, nao wanaitawala hata miili yetu na nyama wetu wa kufuga, kama inavyowapendeza. Kweli sisi tumo katika masongano makubwa.
38Kwa ajili ya haya yote sisi tunafanya agano la kweli, tunaliandika na kulitia muhuri ya wakubwa wetu na ya Walawi wetu na ya watambikaji wetu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.