1Ikawa, mfalme alipokaa nyumbani mwake, kwa kuwa Bwana alikuwa amemtuliza akiwanyamazisha adui zake zote waliomzunguka,
2ndipo, mfalme alipomwambia mfumbuaji Natani: Tazama, mimi ninakaa katika nyumba iliyojengwa kwa miangati, lakini Sanduku la Mungu linakaa katika mapazia tu.Kuomba kwake Dawidi.
18Kisha mfalme Dawidi akaingia pake Bwana, akakaa hapo akisema: Bwana Mungu, mimi ni nani? nao mlango wangu ni nini, ukinileta, nifike hapa?1 Mose 32:10.
19Lakini hayo yakawa madogo machoni pako, Bwana Mungu, kwa hiyo umeyasema yatakayoujia mlango wa mtumishi wako katika siku zilizo mbali bado, hayo nayo umeyasema kimtu, Bwana Mungu.
20Dawidi akuambie nini tena? Maana wewe unamjua mtumishi wako, Bwana Mungu.
21Kwa ajili ya Neno lako na kwa mapenzi ya moyo wako umeyafanya hayo makubwa yote, umjulishe mtumishi wako.
22Kwa hiyo u mkubwa, Bwana Mungu, kwani hakuna anayefanana na wewe, hakuna Mungu, asipokuwa wewe, kwa hayo yote, tuliyoyasikia kwa masikio yetu.
23Tena liko taifa moja tu huku nchini linalofanana na ukoo wako wa Waisiraeli? Hao ndio, Mungu aliokwenda kuwakomboa, wawe ukoo wake, ajipatie Jina kwa kufanya kwao katika nchi yako matendo makubwa yanayoogopesha, ulipofukuza wamizimu na miungu yao mbele yao walio ukoo wako, uliowakomboa, wawe wako, ulipowatoa huko Misri.5 Mose 4:7.
24Ukajiwekea ukoo wako wa Waisiraeli kuwa ukoo wako kale na kale, wewe Bwana ukawa Mungu wao.
25Sasa, Bwana Mungu, neno hilo, ulilolisema la mtumishi wako na la mlango wake, lisimamishe kuwapo kale na kale ukifanya, kama ulivyosema!
26Ndivyo, Jina lako litakavyokuwa kubwa kale na kale kwamba: Bwana Mwenye vikosi ni Mungu wa Isiraeli, tena ndivyo, mlango wa mtumishi wako Dawidi utakavyokuwa wenye nguvu mbele yako.
27Kwani wewe Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, umelifunua sikio la mtumishi wako, asikie ya kwamba: Mimi nitakujengea nyumba. Kwa hiyo mtumishi wako amejipa moyo wa kukuomba maombo haya.Yes. 50:5.
28Sasa Bwana Mungu, wewe ndiwe Mungu; kwa hiyo maneno yako yatatimia kweli, hayo mema, uliyomwambia mtumishi wako, yapate kuwa.
29Sasa na ikupendeze kuubariki mlango wa mtumishi wako, uwepo kale na kale usoni pako! Kwani wewe, Bwana Mungu, umeyasema; kwa hiyo mlango wa mtumishi wako utakuwa umebarikiwa kale na kale kwa kuipata mbaraka yako.*
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.