Waamuzi 18 - Swahili Roehl Bible 1937
Wadani wanakiteka kinyago cha Mika.
1Siku zile hakuwako mfalme kwao Waisiraeli, tena siku zile wao wa shina la Dani walikuwa wanajitafutia fungu la nchi la kukaa, kwani mpaka siku hiyo fungu lao la nchi halijawaangukia katikati ya mashina ya Isiraeli.