Luka 18 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuomba pasipo kuchoka.

1Akawaambia mfano wa kwamba: Imewapasa kuomba siku zote pasipo kuchoka,Fariseo na mtoza kodi.

9*Kulikuwa na watu waliojiwazia wenyewe kuwa waongofu, wakawabeza wengine, akawaambia mfano huu:

10Watu wawili walipanda kwenda Patakatifu kuomba. Wa kwanza alikuwa Fariseo, wa pili mtoza kodi.

11Fariseo akasimama, akaomba na kusema hivi moyoni mwake: Mungu, nakushukuru, kwa sababu sifanani na watu wengine walio wanyang'anyi, wapotovu, wagoni, wala sifanani na huyu mtoza kodi.Kuwabariki watoto.(15-17: Mat. 19:13-15; Mar. 10:13-16.)

15Wakamletea hata vitoto, awaguse. Lakini wanafunzi walipowaona waliwatisha.

16Ndipo, Yesu alipowaita, waje kwake, akisema: Waacheni vitoto, waje kwangu, msiwazuie! Kwani walio hivyo ufalme wa Mungu ni wao.

17Kweli nawaambiani: Mtu asiyeupokea ufalme wa Mungu kama kitoto hatauingia kamwe.Mwenye mali nyingi.(18-30: Mat. 19:16-29; Mar. 10:17-30.)

18Kulikuwa na mkubwa, akamwuliza akisema: Mfunzi mwema, nifanye nini, niurithi uzima wa kale na kale?

19Yesu akamwambia: Unaniitaje mwema? Hakuna aliye mwema, asipokuwa Mungu peke yake tu.

20Maagizo unayajua, ya kwamba: Usizini! Usiue! Usiibe! Usisingizie! Mheshimu baba yako na mama yako!Mwana wa mtu atateswa.(31-34: Mat. 20:17-19; Mar. 10:32-34.)

31*Akawatwaa wale kumi na wawili, akawaambia: Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu. Huko Mwana wa mtu aliyoandikiwa na wafumbuaji yatatimizwa yote:Kipofu wa Yeriko.(35-43: Mat. 20:29-34; Mar. 10:46-52.)

35Ikawa, alipokaribia Yeriko, palikuwa na kipofu aliyekaa njiani kando akiomba sadaka.

36Aliposikia, kundi la watu linapita, akauliza: Kuna nini?

37Wakamsimulia, ya kuwa Yesu wa Nasareti anapita.

38Ndipo, alipopaza sauti akisema: Yesu, mwana wa Dawidi, nihurumie!

39Wao waliotangulia walipomkaripia, anyamaze, yeye akakaza sana kupaza sauti: Mwana wa Dawidi, nihurumie!

40Ndipo, Yesu aliposimama, akaagiza, aletwe kwake. Alipomfikia, akamwuliza:

41Wataka, nikufanyie nini? Naye akasema: Bwana, nataka, nipate kuona.

42Yesu akamwambia: Ona! Kunitegemea kwako kumekuponya.Luk. 17:19.

43Papo hapo akapata kuona, akamfuata akimtukuza Mungu. Nao watu wote walioviona wakamsifu Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help