1Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote, nitayasimulia mataajabu yako, uliyoyafanya yote.
2Kwa kufurahi nitakushangilia, nitaliimbia Jina lako wewe ulioko huko juu,
3kwani adui zangu wamerudi nyuma, wakajikwaa, wakaangamia machoni pako.
4Maana umenipatia kushinda, nilipohukumiwa, ukakalia kiti cha uamuzi, utoe hukumu iongokayo.
7Bwana hukaa kale na kale, akakisimika kiti chake, atoe hukumu.
15Wamizimu wamedidimia katika shimo, walilolifanya wao, miguu yao ikanaswa katika tanzi, walilolitega wenyewe.
19Inuka, Bwana, watu wasikaze nguvu, wamizimu wahukumiwe machoni pako!
20Wakemee wamizimu, Bwana, kusudi wastushwe, kusudi wajitambue kuwa watu tu!
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.