Mateo 15 - Swahili Roehl Bible 1937

Maagizo ya Mungu na mazoea ya watu.(1-20: Mar. 7:1-23.)

1Ndipo, walipomjia Yesu Mafariseo na waandishi waliotoka Yerusalemu, wakasema:

8Ukoo huu huniheshimu kwa midomo tu,

lakini mioyo yao inanikalia mbali.

9Hivyo hunicha bure,

kwani hufundisha mafundisho yaliyto maagizo ya watu tu.

10Akaliita kundi la watu, akawaambia: Sikilizeni, mjue maana!

11Kinachoingia kinywani sicho kinachomtia mtu uchafu, ila kinachotoka kinywani ndicho kinachomtia mtu uchafu.

12Ndipo, wanafunzi walipomjia, wakamwuliza: Unajua, ya kuwa Mafariseo walikwazwa walipolisikia neno hilo?

13Naye akajibu akisema: Kila mmea, asioupanda Baba yangu wa mbinguni, utang'olewa.

14Waacheni hao! Ni mapofu wenye kuongoza vipofu wenzao. Kipofu akimwongoza kipofu mwenziwe, wote wawili watatumbukia shimoni.Kuponya wagonjwa wengi.

29Kisha Yesu akaondoka huko, akafika kandokando ya bahari ya Galilea, akapanda mlimani, akakaa huko.Watu 4000 wanalishwa.(32-39: Mar. 8:1-10.)

32Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema: Kundi hili la watu nalionea uchungu, kwa kuwa wameshinda kwangu siku tatu, wasione chakula. Nami sitaki kuwaaga, waende zao pasipo kula, maana wasije, wakazimia njiani.Mat. 14:14.

33Wanafunzi wakamwambia: Hapa nyikani tutapata wapi mikate inayotosha kuwashibisha watu walio wengi kama hawa?

34Yesu akawauliza: Mnayo mikate mingapi? Nao waliposema: Tunayo saba na visamaki vichache,

35akawaagiza hao watu wengi, wakae chini.

36Kisha akaitwaa ile mikate saba na samaki, akashukuru, akaimega akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawapa wao wa makundi ya watu.

37Wote wakala, wakashiba; kisha wakayaokota makombo ya mikate yaliyosalia, wakajaza makanda saba.

38Nao waliokula walikuwa waume tu 4000 pasipo wanawake na watoto.

39Kisha akawaaga makundi, waende zao, akaingia chomboni, akaja mipakani kwa Magadala.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help