1Agripa alipomwambia Paulo: Una ruhusa kujisemea mwenyewe, ndipo, Paulo aliponyosha mkono, akajikania hivyo:
2Mfalme Agripa, ninashangilia moyoni, kwa kuwa yote, ninayosutwa na Wayuda, nitajikania leo mbele yako wewe,
3uliyeyatambua sanasana mazoea na mashindano yote ya Kiyuda. Kwa hiyo nakuomba, unisikilize kwa kuvumilia.
4Mwendo wangu ulivyokuwa hapo mwanzo, nilipokuwa kijana pamoja na vijana wenzangu huko Yerusalemu, Wayuda wote wanavijua.
5Kwani wamenitambua kale; wakitaka wangenishuhudia, ya kwamba nimekifuata kile chama kinachokaza kuyashika mambo ya tambiko letu, kwani nalikuwa Fariseo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.