Luka 22 - Swahili Roehl Bible 1937

Yuda Iskariota.(1-2: Mat. 26:1-5; Mar. 14:1-2.)

1Ikawa karibu sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, inayoitwa Pasaka.

2Nao watambikaji wakuu na waandishi wakatafuta, ndivyo wapate kumwangamiza. Maana walikuwa wakiwaogopa watu wa kwao.(3-6: Mat. 26:14-16; Mar. 14:10-11.)

3Satani akamwingia Yuda anayeitwa Iskariota, naye alikuwa mwenzao wale kumi na wawili.Chakula cha Bwana.

14*Saa ilipofika, akaja kukaa chakulani, nao mitume wakakaa pamoja naye.

15Akawaambia: Nimetunukia sanasana kuila Pasaka hii pamoja nanyi, nikingali sijateswa bado.

16Kwani nawaambiani: Sitaila tena, mpaka patakapotimia katika ufalme wa Mungu.Simoni Petero.(31-34: Mat. 26:31-35; Mar. 14:27-31; Yoh. 13:36-38.)

31Simoni, Simoni, tazama, Satani amewataka ninyi, awapepete, kama wanavyopepeta ngano!Kukana kwa Petero.(54-62: Mat. 26:57,58,69-75; Mar. 14:53,54,66-72; Yoh. 18:12-18, 25-27.)

54*Walipokwisha kumkamata, wakampeleka, wamwingize nyumbani mwa mtambikaji mkuu. Lakini Petero akafuata mbalimbali.

55Walipowasha moto katikati ya ua na kukaa pamoja, naye Petero akaja kukaa katikati yao.

56Kijakazi alipomwona, akikaa penye mwangaza wa moto, akamkazia macho, akasema: Hata huyu alikuwa pamoja naye.

57Akakana akisema: Simjui, mama.

58Punde kidogo mwingine akamwona, akasema: Wewe nawe u mwenzao. Lakini Petero akasema: Mwenzangu, siye mimi.

59Saa moja ilipopita, mwingine akakaza kusema: Kweli hata huyu alikuwa pamoja naye, kwani ni Mgalilea.

60Lakini Petero akasema: Mwenzangu, sijui, unavyosema. Angali akisema, papo hapo jogoo akawika.

61Ndipo, Bwana alipomgeukia Petero, amtazame; hapo Petero akalikumbuka lile neno la Bwana, kama alivyomwambia: Jogoo atakapokuwa hajawika leo, utakuwa umenikana mara tatu.Luk. 22:34.

62Akatoka nje, akalia sana kwa uchungu.*

Yesu anafyozwa.(63-65: Mat. 26:67-68; Mar. 14:65.)

63*Wale waume waliomshika Yesu wakamfyoza na kumpiga,

64wakamfunika uso, wakamwuliza wakisema: Fumbua! Ni nani aliyekupiga?

65Hata masimango mengine mengi wakasema na kumtukana.

Mwana wa Mungu(66-71: Mat. 26:59-66; Mar. 14:55-64.)

66Kulipokucha, wakakusanyika wazee wa kwao na watambikaji wakuu na waandishi, wakampeleka barazani kwa wakuu wao wote.Yoh. 18:24.

67Wakasema: Tuambie, kama wewe ndiwe Kristo! Akawaambia: Nikiwaambia, hamtanitegemea;

68lakini nikiwauliza, hamtanijibu, wala hamtanifungua.

69Lakini tangu sasa Mwana wa mtu atakuwa amekaa kuumeni kwa nguvu ya Mungu.Sh. 110:1.

70Ndipo, waliposema wote: Je? Ndiwe mwana wa Mungu? Naye akawaambia: Ninyi mnasema, kwani nimi ndiye.

71Nao wakasema: Ushuhuda tunautakia nini tena? Kwani wenyewe tumevisikia, anavyosema.*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help