1Aburahamu akaoa tena, jina lake mkewe ni Ketura.Vizazi vya Isimaeli.
12Hivi ndiyo vizazi vya Isimaeli, mwana wa Aburahamu, ambaye Hagari wa Misri aliyekuwa kijakazi wake Sara alimzalia Aburahamu.Kuzaliwa kwao Esau na Yakobo.
19Hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Aburahamu: Aburahamu alimzaa Isaka.
20Isaka alikuwa mwenye miaka 40 alipomchukua Rebeka kuwa mkewe, naye alikuwa binti Betueli, Mshami na Mesopotamia, dada yake Mshami Labani.
21Isaka akamwombea mkewe kwake Bwana, kwani alikuwa mgumba; naye Bwana akayaitikia maombo yake, ndipo, mkewe Rebeka alipopata mimba,
22Watoto walipogongana tumboni mwake, akasema: Kama ndivyo, nimevipatia nini? Akaenda kumwuliza Bwana.
23Bwana akamwambia:
Mataifa mawili yamo tumboni mwako,
kabila mbili za watu zinatengana tumboni mwako
zikitaka kutoka,
kabila moja itatenda nguvu kuishinda ile nyingine,
naye mkubwa atamtumikia nduguye.
24Siku zake za kuzaa zilipotimia, ikaonekana, ya kuwa wana wa pacha wamo tumboni mwake.
25Wa kwanza alipotoka alikuwa mwekundu, mwenye manyoya mwilini mote kama vazi la ngozi, wakamwita jina lake Esau.
26Ndugu yake alipotoka baadaye, mkono wake ulikuwa unakishika kisigino cha Esau, wakamwita jina lake Yakobo. Naye Isaka alikuwa mwenye miaka 60, mkewe alipowazaa.
27Hawa watoto walipokua, Esau akawa wa porini na fundi wa kuwinda, lakini Yakobo akawa mtulivu, akapenda kukaa hemani.
28Kwa hiyo Isaka akampenda Esau, kwa kuwa alimpatia nyama za kula za porini, lakini Rebeka alikuwa anampenda Yakobo.
Esau anamwuzia Yakobo ukubwa wake.29Siku moja Yakobo alipopika kunde, Esau akarudi toka porini, naye alikuwa amechoka sana.
30Ndipo, Esau alipomwambia Yakobo: Nipe, nile upesi hicho chekunduchekundu! Kwani nimechoka sana. Kwa sababu hii wakaliita jina lake Edomu (Mwekundu).
31Lakini Yakobo akasema: Niuzie leo hivi ukubwa wako!
32Naye Esau akasema: Tazama, mimi ninakwenda kufa! Hapo ukubwa utanifaa nini?
33Yakobo akasema: Uniapie leo hivi! Basi, akamwapia; hivyo ndivyo, alivyomwuzia Yakobo ukubwa wake.1 Mose 27:36; Ebr. 12:16.
34Kisha Yakobo akampa mkate na hizo kunde, alizozipika; naye akala, akanywa, kisha akainuka, akaenda zake. Hivyo ndivyo, Esau alivyoubeza ukubwa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.