1Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Noa: Semu, Hamu na Yafeti; nao walizaliwa wana baada ya mafuriko ya maji.
2Wana wa Yafeti ni Gomeri na Magogi na Madai na Yawani na Tubali na Meseki na Tirasi.
3Nao wana wa Gomeri ni Askenazi na Rifati na Togarma.
4Nao wana wa Yawani ni Elisa na Tarsisi na Wakiti na Wadodani.
5Kwao hao walijitenga wenyeji wa visiwa vya wamizimu, wakae katika nchi zao, kila kabila lenye msemo wake; hivyo ndivyo, koo zao zilivyopata kuwa mataifa.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.