Mashangilio 31 - Swahili Roehl Bible 1937

Maombo ya mtu amtegemeaye Bwana hata siku za mahangaiko.Kwa mwimbishaji. Wimbo wa Dawidi.

1Wewe Bwana, nimekukimbilia, sitatwezeka kale na kale. Kwa kuwa mwenye wongofu na uniponye!

2Nitegee sikio lako, unisaidie upesi! Niwie mwamba wenye nguvu na nyumba yenye boma! Ndivyo, utakavyopata kuniokoa.

9Niwie mpole, Bwana! Kwani nimesongeka, macho yangu yamenyauka kwa uchungu, nayo roho vilevile pamoja na mwili.

14Lakini mimi ninayemwegemea, ndiye Bwana, Mungu wangu ndiwe wewe! Hii naungama.

15Mikononi mwako ndimo, siku zangu za kuwapo zilimo; niponye na kunitoa mikononi mwao adui zangu wanikimbizao!

17Bwana, usiniache, nisije kutwezwa, kwani nikakulilia; sharti watwezwe wao wasiokucha, na waje kuzimuni kuyamazia huko!

18Midomo yenye uwongo sharti ifumbwe kuwa kimya, kwani mwongofu wamemtolea meneno ya kumkorofisha, kwa majivuno yao wakambeza.

19Ninayastaajabu mema yako, jinsi yalivyo mengi, umeyalimbikia wao wakuogopao, nao wakukimbiliao huwapa machoni pa watu.

20Mafichoni kwa uso wako unawaficha, watu wakiwatolea ukali; ukawafunika chumbani ndani, ndimi zao zikiwagombeza.

21Bwana na atukuzwe! Kwani amenistaajabisha, akaniweka mjini mwenye nguvu kwa upole wake.

23Mpendeni Bwana, ninyi yote mmchao! Bwana huwalinda wamtegemeao. Lakini wafanyao majivuno huwalipisha, asisaze hata kidogo.

24Jipeni mioyo, mpate nguvu, nyote mnaomngojea yeye Bwana!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help