Mateo 23 - Swahili Roehl Bible 1937

Kuwatisha waandishi na Mafariseo.(1-39: Mar. 12:38-40; Luk. 11:39-52; 20:45-47.)

1Kisha Yesu akasema na watu waliokutanika na wanafunzi wake,

2kwamba: Kitini pa Mose wamekaa waandishi na Mafariseo.

3Yo yote, watakayowaambia, yafanyeni na kuyashika! Lakini kama wafanyavyo, msiyafuate! Kwani kusema wanasema, lakini hawayafanyi.

23Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani fungu la kumi mnalitolea hata mchicha na nyanya na pilipili, lakini yaliyo magumu katika Maonyo mmeyaacha, yale ya hukumu na ya huruma na ya mategemeo. Haya yawapasa kuyashika pasipo kuyaacha yale.

34*Kwa sababu hii tazameni, mimi natuma kwenu wafumbuaji na werevu wa kweli na waandishi; wengine wao mtawaua na kuwawamba misalabani, wengine wao mtawapiga katika nyumba zenu za kuombea, kisha mtawafukuza mji kwa mji;

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help