Waroma 7 - Swahili Roehl Bible 1937

Nguvu ya Maonyo.

1Na niseme nanyi, kwa kuwa mnayatambua Maonyo: Hamjui, ndugu: Maonyo humshika mtu siku zote za maisha yake?

2Kwani mwanamke aliye na mume siku za kuishi kwake mumewe ana mwiko kwa ajili ya Maonyo; lakini nguvu ya hayo Maonyo hukoma, mumewe anapokufa, hana mwiko tena wa mwanamume mwingine.

3Siku za kuishi kwake mumewe, yeye akiwa wa mume mwingine, huitwa mzinzi. Lakini mumewe anapokufa, amefunguliwa na Maonyo, asiwe tena mzinzi akiwa wa mume mwingine.

4Ndugu zangu, hapo Kristo alipokufa, mliuawa nanyi, mkayafia Maonyo; kwa hiyo mmefunguliwa nanyi kuwa wa mwingine, maana ni wa yule aliyefufuliwa katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.

7*Sasa tusemeje? Maonyo hukosesha? La, sivyo! Lakini kosa singelitambua pasipo Maonyo. Kwani hata tamaa singeijua, kama Maonyo yasingesema: Usitamani!Utumwa wa ukosaji.

13Basi, inakuwaje? Lililo jema ndio lililoniua mimi? La, sivyo! Ila ukosaji ndio ulioniua; lakini kusudi uonekane kuwa ukosaji, ukaniua kwa lile lililo jema; kwa hivyo, ukosaji ulivyolitumia lile agizo, ukatokea wazi kuwa ukosaji wenyewe usiozuilika kabisa.

24Yamenipata mimi mtu mkiwa! Yuko nani atakayenikomboa utumwani mwa mwili huu wa kufa?

25Mungu atolewe shukrani kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Basi, kwa akili zangu mimi mwenyewe nayatumikia kitumwa Maonyo yake Mungu, lakini mwilini ni mtumwa wa maonyo ya ukosaji.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help