Ezekieli 14 - Swahili Roehl Bible 1937

Wanaotumikia vinyago hawajibiwi na Mungu.

1Wakaja kwangu waume wazee wa Kiisiraeli, wakakaa mbele yangu.Mapatilizo ya Yerusalemu hayana budi kutimia, lakini wako watakaosazwa.

12Neno la Bwana likanijia la kwamba:Ez. 5:16.

13Mwana wa mtu, nchi ikinikosea na kuvunja maagano, nitaikunjulia mkono wangu, nilivunje shikizo lao la chakula na kuipelekea njaa, nimalize huko watu na nyama.

14Lakini kama wangekuwako katika ile nchi watu hawa watatu: Noa na Danieli na Iyobu, hawa wangejiponya kwa wongofu wao; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.Yer. 15:1.

15Kama ningeleta nyama wabaya, watembee katika ile nchi na kuwamaliza watu walioko, iwe peke yake, asipite mtu kwa ajili ya wale nyama,Ez. 14:21.

16basi, kama wangekuwako katika ile nchi hao watu watatu: hivyo, nilivyo Mwenye uzima, ndivyo, Bwana Mungu asemavyo, nao hawataponya wana wa kiume wala wa kike, ila wangepona wao wenyewe tu, hiyo nchi iwe peke yake.

17Au kama ningeiletea ile nchi panga nikisema: Panga na zitembee katika nchi hii, nitoweshe kwake watu na nyama,

18kama wangekuwako katika ile nchi hao watu watatu: hivyo, nilivyo Mwenye uzima, ndivyo, Bwana Mungu asemavyo, hawataponya wana wa kiume waka wa kike, ila wangepona wao wenyewe tu.

19Au kama ningeipelekea ile nchi magonjwa mabaya, akiimwagia makali yangu yenye moto pamoja na kumwaga damu, nitoweshe kwake watu na nyama,

20kama wangekuwako katika ile nchi Noa na Danieli na Iyobu: hivyo, nilivyo Mwenye uzima, ndivyo, asemavyo Bwna Mungu, hawataponya mwana wa kiume wala wa kike, ila wengepona wao wenyewe tu kwa wongofu wao.

21Kwani hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Ingawa niupelekee Yerusalemu haya mapatilizo yangu manne yaliyo mabaya: panga na njaa na nyama wabaya na magonjwa mabaya, nitoweshe mwake watu na nyama,3 Mose 6:16-25; Yer. 15:3.

22mtaona, wakisazwa mwake waliopona watakaohamishwa wa kiume na wa kike, hao mtawaona wakitokea kwenu, mzitazama njia zao na matendo yao; ndipo, mtakapoituliza mioyo yenu kwa ajili ya mabaya, niliyouletea Yerusalemu, na kwa ajili yao yote, niliyouletea.

23Wataituliza mioyo yenu, mtakapozitazama njia zao na matendo yao; ndipo, mtakapojua, ya kuwa sikuyafanya bure tu hayo yote, niliyoufanyia; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help