Ufunuo 12 - Swahili Roehl Bible 1937

Mwanamke na joka.

1Kisha kukaonekana kielekezo kikubwa mbinguni: mwanamke aliyekuwa amevikwa jua alikuwa anao mwezi chini miguuni pake, napo kichwani pake alikuwa na kilemba cha nyota kumi na mbili.

2Kwa kuwa ana mimba, akalia kwa kuona uchungu na maumivu ya kuzaa.Joka wa kale anashindwa na kutupwa.

7Kukawa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakaja kupigana na yule joka; yule joka na malaika zake walipopiga vita,Dan. 10:13,21; 12:1.

8hawakushinda, tena hapakuonekana mahali pao pa kukaa mbinguni.

9Kisha yule joka kubwa akabwagwa nchini, ni yule nyoka wa kale aitwaye Msengenyaji na Satani aliyeupoteza ulimwengu wote, akabwagwa nchini, nao malaika zake wakabwagwa pamoja naye.1 Mose 3:1,14; Luk. 10:18; Yoh. 12:31.

10Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema:

Sasa wokovu na uwezo na ufalme umekuwa wa

Mungu wetu, nazo nguvu zimekuwa zake Kristo

wake, kwani msutaji wa ndugu zetu amebwagwa nchini;

ndiye aliyewasuta mbele ya Mungu

wetu mchana na usiku.Ufu. 11:15; Iy. 1:11; Zak. 3:1; Luk. 22:31.

11Nao wamemshinda kwa

nguvu ya damu ya Mwana kondoo na kwa

nguvu ya neno la ushahidi wao. Nao hawakujipenda

wenyewe mpaka kufa.Ufu. 6:9; 7:14; 12:17; Rom. 8:37.

12Kwa hiyo shangilieni,

enyi mbingu nanyi mkaao mwake! Lakini ninyi nchi na

bahari, yatawapata! Kwani Msengenyaji ameshuka kwenu

ninyi mwenye makali mengi moyoni, kwani ajua, ya kuwa

siku zake ni chache tu.

Makali ya joka.

13Yule joka alipoona, ya kuwa amebwagwa nchini, ndipo, alipomkimbiza yule mwanamke aliyemzaa yule mtoto wa kiume.

14Lakini mwanamke akapewa mabawa mawili ya yule tai mkibwa, aende nyikani na kuruka, apafikie mahali pake, anapolishwa siku hizi nazo zitakazokuja nacho kipande cha siku zitakazosalia, atoke usoni pake yule joka.Ufu. 12:6; Dan. 7:25; 12:7.

15Ndipo, yule joka alipotoa maji kinywani mwake kama mto, akamtemea yule mwanamke kwamba amtose mle mtoni.

16Lakini nchi ikamsaidia yule mwanamke, maana hiyo nchi ikakifumbua kinywa chake, ikaunywa ule mto, yule joka alioutoa kinywani mwake.

17Kwa hiyo yule joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake kufanya vita nao waliosalia wa uzao wake, ndio wale walioyashika maagizo yake Mungu, waliofuliza kumshuhudia Yesu.Ufu. 14:12; 19:10; Ebr. 11:2; 1 Yoh. 5:10.

18Kisha nikapelekwa kusimama ufukoni penye bahari.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help