Ezekieli 8 - Swahili Roehl Bible 1937
Matapisho ya kutambikia vinyago Patakatifu pa Bwana.
1Ikawa katika mwaka wa sita siku ya tano ya mwezi wa sita nilipokuwa nimekaa nyumbani mwangu pamoja na wazee wa Yuda waliokaa mbele yangu, ndipo, mkono wa Bwana Mungu uliponiangukia.