Danieli 5 - Swahili Roehl Bible 1937

Penye karamu ya Belsasari yanaandikwa ukutani maneno yasiyosomeka.

1Mfalme Belsasari aliwafanyia wakuu wake elfu karamu kubwa, akanywa mvinyo mbele yao hao elfu.Danieli anayafumbua yale maandiko.

13Kisha Danieli akapelekwa mbele yake mfalme, mfalme akamwuliza Danieli akisema: Wewe ndiwe Danieli, mmoja wao Wayuda, baba yangu mfalme aliowateka na kuwahamisha kuja huku akiwatoa katika nchi ya Yuda?

14Nimesikia habari zako, ya kuwa roho ya miungu imo mwako, kwa hiyo mwako unaoneka mwangaza na utambuzi na ujuzi mwingi sana!

15Sasa hapa wajuzi na waaguaji wameletwa mbele yangu, wayasome maandiko haya, wanijulishe maana yake, lakini hawawezi kuifumbua maana yake hilo jambo.

16Lakini habari zako wewe nimesikia, ya kuwa unaweza kusema maana na kuyavumbua yaliyofunikwa; basi, kama unaweza kuyasoma maandiko haya na kunijulisha maana yao, utavikwa nguo za kifalme, napo shingoni pako utapata mkufu wa dhahabu, tena utakuwa mwenye kutawala wa tatu katika ufalme.

17Kisha Danieli akamjibu mfalme akisema: Kaa na vipaji vyako! Umpe mwingine matunzo yako! Lakini haya maandiko nitamsomea mfalme, nayo maana yao nitamjulisha.

18Wewe mfalme, Mungu Alioko huko juu alimpa baba yako Nebukadinesari ufalme na ukuu na enzi na utukufu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help