1Rubeni, mwana wa kwanza wa Isiraeli, alikuwa kweli mzaliwa wake wa kwanza; lakini kwa kuwa aliyachafua malalo ya baba yake, uzaliwa wake wa kwanza walipewa wana wa Yosefu, mwana wa Isiraeli, ingawa hawakuandikiwa uzaliwa wa kwanza katika kitabu cha udugu.
18Wana wa Rubeni na wa Gadi nao wa nusu ya shina la Manase, wao waliokuwa wenye nguvu, walioweza kushika ngao na panga, waliojua kuvuta pindi, waliofundishwa vita, walikuwa watu 44760; ndio waliotoka kwenda vitani,
19wakapigana nao Wahagri nao Wayeturi nao Wanafisi nao Wanodabu.
20Wakasaidiwa kuwashinda, nao Wahagri pamoja nao wote waliokuwa pamoja nao wakatiwa mikononi mwao, kwani walimlilia Mungu katika mapigano, naye akayasikia maombo yao, kwa kuwa walimtegemea.
21Wakayateka makundi yao: ngamia 50000, mbuzi na kondoo 250000 na punda 2000 na watu 100000.
22Kwani walioumizwa walianguka wengi, kwa kuwa vita hivyo vilikuwa vimetoka kwake Mungu, wakakaa mahali pao, mpaka walipotekwa na kuhamishwa.
Vizazi vya nusu ya Manase.23Nao wana wa nusu ya shina la Manase walikaa katika nchi hiyo toka Basani mpaka Baali-Hermoni, tena mpaka Seniri na milimani kwa Hermoni, nao walikuwa wengi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.