Mashangilio 91 - Swahili Roehl Bible 1937

Kumngojea Bwana ni kuzuri.

1Akaaye fichoni kwake alioko huko juu, alalaye kivulini kwake aliye Mwenyezi

2humwambia Bwana: Kimbilio langu, tena ngome yangu, Mungu wangu, nimwegemeaye!

3Kwani yeye ndiye aniokoaye tanzini mwa mwindaji, namo mwenye kipindupindu kiangamizacho.

9Kwani wewe ulisema: Bwana ni kimbilio langu, naye Alioko huko juu unamtumia kuwa kao lako.

10Hakuna kibaya kitakachokufikia mwako nyumbani, wala hakuna pigo litakalokikaribia kituo chako.

11Kwani atakuagizia malaika zake, wakulinde katika njia zako ziwazo zote.

14Kwa kuwa ameshikamana na mimi, nitamwopoa, kwa kuwa analijua Jina langu, nitamkweza.

15Atakaponiita, nitamwitikia, mimi niko pamoja naye katika masongano, nimwokoe, kisha nimpe hata utukufu.

16Wingi wa siku zake za kuwapo ndio, nitakaomshibisha, nimchangamshe, akiuona huo wokovu wangu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help