1Hivi ndivyo, Bwana Mungu anavyosema: Lango la ua wa ndani lielekealo maawioni kwa jua sharti liwe limefungwa siku sita za kazi, lakini siku ya mapumziko lifunguliwe, hata siku ya mwandamo wa mwezi lifunguliwe.
2Mkuu akiingia penye ukumbi wa hilo lango toka nje, asimame hapo penye mhimili wa hilo lango, watambikaji waitengeneze ng'ombe yake ya tambiko ya kuteketezwa nzima nazo ng'ombe za tambiko za kushukuru, naye amwangukie Mungu penye kizingiti cha hilo lango, kisha atoke; kisha lango hilo lisifungwe mpaka jioni.Majiko ya kutengenezea ng'ombe na vilaji vya tambiko.
19Akanipeleka hapo pa kuingia palipokuwa kando ya lile lango la kuviingilia vile vyumba vitakatifu vya watambikaji vielekeavyo kaskazini; hapo nikaona mahali pembeni panapoelekea baharini.
20Akaniambia: Humu ndimo, watambikaji wanamopikia nyama za ng'ombe za tambiko za upozi nazo za weuo, tena ndimo, wanamochomea vilaji vya tambiko, kusudi wasivipeleke katika ua wa nje na kuwapatia watu utakatifu.
21Kisha akanitoa na kunipeleka katika ua wa nje, akanipitisha penye pembe zake nne za huo ua; ndipo, nilipoona penye kila pembe ya huo ua ua mwingine.
22Penye pembe zote nne za huo ua palikuwa na nyua zilizofungwa kwa ukuta, urefu wao ulikuwa mikono 40, nao upana 30, kipimo chao hizo nyua ni kimoja tu.
23Zote nne zilizungukwa na ukuta wa mawe; chini penye hizo kuta kuzizunguka zote palikuwa pametengenezwa majiko.
24Akaniambia: Hizi ndizo nyumba za wapishi, watumishi wa Nyumba hii walimopikia nyama za ng'ombe za tambiko za watu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.