Luka 7 - Swahili Roehl Bible 1937

Mkubwa wa Kapernaumu.(1-10: Mat. 8:5-13.)

1Alipokwisha kuyasema maneno yake yote, watu wakimsikiliza, akaenda, akaingia Kapernaumu.

2Kukawako mkubwa wa askari mwenye mtumwa, ambaye alipendezwa sana naye; huyu alikuwa mgonjwa wa kufa.

3Bwana wake aliposikia mambo ya Yesu akatuma kwake wazee wa Wayuda, wamwombe, aje, amponye mtumwa wake.

4Walipomfikia Yesu wakakaza kumbembeleza wakisema: Amepaswa, umfanyie hivyo;

5kwani anatupenda sisi taifa letu, hata nyumba ya kuombea ametujengea mwenyewe.

6Yesu akaenda pamoja nao; alipokuwa mbali kidogo kuifikia ile nyumba, yule mkubwa wa askari akatuma rafiki zake kumwambia: Bwana, usijisumbue! Kwani hainipasi, uingie kijumbani mwangu.

7Kwa hiyo nami sikujipa moyo wa kukujia mwenyewe. Ila sema neno tu! ndipo, mtoto wangu atakapopona!

8Kwani nami ni mtu mwenye kuitii serikali, ninao askari chini yangu. Nami nikimwambia huyu: Nenda! basi, huenda; na mwingine: Njoo! huja; nikimwagiza mtumishi wangu: Vifanye hivi! huvifanya.

9Yesu alipoyasikia hayo akamstaajabu, akaligeukia kundi la watu lililomfuata, akasema: Nawaambiani, hata kwa Waisiraeli sijaona bado mwenye kunitegemea kama huyu.

10Wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa, yuko amepona.

Kijana wa Naini.

11*Kisha punde kidogo akashika njia kwenda katika mji, jina lake Naini. Wakafuatana naye wanafunzi wake na kundi la watu wengi.

12Alipolikaribia lango la mji, panatolewa mfu; huyu alikuwa mwana wa pekee wa mama yake, naye alikuwa mjane. Kwa hiyo watu wengi wa mji ule walikwenda pamoja naye.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help