1Mimi Paulo niliye mtume wa Kristo Yesu kwa hayo, Mungu ayatakayo, na ndugu TimoteoUtukufu wa Utume.
21Hata ninyi kale mlikuwa wageni naye, mkawa hata wachukivu wake, maana mioyoni mlifuata matendo mabaya.Rom. 5:10; Ef. 2:12-13; 4:18.
22Lakini sasa amewapatanisha hata ninyi hapo, alipokufa na kuutoa mwili wake wa kimtu, awageuze nanyi kuwa machoni pake watakatifu pasipo kilema wala kosa.Ef. 5:27.
23Mtakuwa hivyo mkifuliza kumtegemea, kwani mmajengwa juu ya msingi wenye nguvu, msiwezekane kuondolewa penye kingojeo cha Utume mwema, mliousikia; ndio unaotangaziwa kila kiumbe kilichoko chini ya mbingu. Nami Paulo ninautumikia.
24Sasa nafurahiwa nayo mateso, niliyoyapata kwa ajili yenu. Nayo maumivu, Kristo aliyoyasaza, nayatimiliza katika mwili wangu, unapoteswa kwa ajili ya mwili wake, maana wateule wake.Ef. 3:13; 2 Tim. 2:10.
25Ndio wao, niwatumikiao nikiufuata utunzaji wa Mungu, niliopewa, niwatimilizie ninyi Neno lake Mungu.
26Ni lile fumbo lililokuwa limefichwa tangu kale, baba wasilijue. Lakini sasa watakatifu wake wamekwisha kufumbuliwa;Rom. 16:25-26; Ef. 1:9-10; 3:4-9; 1 Tim. 3:16.
27kwani ndio, Mungu aliotaka kuwatambulisha, limbuko likuavyo, lile la utukufu wa fumbo hili, awalimbikialo wamizimu, ndilo hili: Kristo yumo mwenu, yeye ndio utukufu unaongojewa.1 Tim. 1:1.
28Naye ndiye, tunayemtangaza sisi, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu werevu wote ulio wa kweli, tupate kumgeuza kila mtu kuwa mtimilifu kwa nguvu ya Kristo.Kol. 1:22.
29Kazi hii ndiyo, niisumbukiayo na kuishindania kwa uwezo wake yeye anayeniwezesha hivyo kwa nguvu yake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.