1Kisha Yosia akamfanyia Bwana huko Yerusalemu sikukuu ya Pasaka, wakachinja wana kondoo wa Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.
2Akawaagiza watambikaji kuja kuzifanya kazi zao ziwapasazo, akawashikiza mioyo, watumikie Nyumbani mwa Bwana.
3Akawaambia Walawi waliowafundisha Waisiraeli wote, waliokuwa watakatifu wa Bwana: Liwekeni Sanduku takatifu katika hiyo Nyumba, aliyoijenga Salomo, mwana wa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli! Msilichukue tena mabegani! Sasa mtumikieni Bwana Mungu wenu, mwatumikie nao walio ukoo wake,
16Ndivyo, kazi zote za utumishi wa Bwana zilivyotengenezwa siku ile ya kufanya Pasaka pamoja na kuteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa kumtambikia Bwana, kama mfalme Yosia alivyoagiza.
17Nao wana wa Isiraeli waliokuwako wakafanya Pasaka siku hiyo, nayo hiyo sikukuu ya Mikate isiyochachwa wakaila siku saba.
18Pasaka kama hii haikufanywa kwa Waisiraeli tangu siku za mfumbuaji Samweli; wafalme wote wa Waisiraeli hawakufanya Pasaka, kama Yosia alivyoifanya pamoja na watambikaji na Walawi na Wayuda na Waisiraeli wote waliokuwako na wenyeji wa Yerusalemu.
26Mambo mengine ya Yosia na matendo ya upole wake yaliyopatana nayo yaliyoandikwa katika Maonyo ya Bwana,
27nayo mambo yake ya kwanza na ya mwisho tunayaona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Waisiraeli na wa Wayuda.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.