Mashangilio 90 - Swahili Roehl Bible 1937

Kitabu cha nne.(Sh. 90—106.)Mungu ni kimbilio letu.Maombo ya Mose aliyekuwa mtu wake Mungu.

1Bwana, wewe ndiwe kimbilio letu kwa vizazi na vizazi.

2Milima ilipokuwa haijazaliwa bado, hata nchi na ulimwengu zilipokuwa hazijaumbwa bado, wewe Mungu ulikuwa uko tangu kale hata kale.

3Unawageuza watu kuwa mavumbi tena ukiwaambia: Rudini, ninyi wana wa watu!

11Lakini yuko nani azitambuaye nguvu za makali yako? Tena yuko nani ayaogopaye hayo machafuko yako?

12Tufundishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie mioyo yenye ujuzi!

13Rudi, Bwana! Utatukalia mbali mpaka lini? Walio watumishi wako wahurumie!

14Tushibishe upole wako kila kunapokucha! Ndivyo, tutakavyoshangilia kwa furaha siku zetu zote.

15Siku za kutufurahisha ziwe sawasawa nazo, ulizotutesa, ziwe miaka mingi, kama ilivyokuwa ile ya kuona mabaya.

16Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, nao utukufu wako kwa wana wao!

17Nao wema wake Bwana Mungu wetu na utukalie! Kazi za mikono yetu zifanikishe kwetu! Kazi za mikono yetu uzifanikishe kweli!*

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help